Ni kitu cha kujivunia katika
jamii yetu ya kitanzania kuwa na taasisi mbalimbali zinazotoa mchango mkubwa
katika kukuza ujasiriamali wa ndani zikiwemo zile zinazotoa mikopo nafuu
kwaajiri ya wajasiriamali wadogo taasisi
za aina hii ni pamoja na SACCoS, FINCA, Na nyinginezo , lakini pia zipo
nyingine zinazotoa misaada katika kusaidia kuwezesha miradi mikubwa ya
ujasiriamali katika nchi yetu ya Tanzania kama vile taasisi zisizo za
kiserikali (NGO’s) mfano Trias, na BESTAC
lakini pia zipo taasisi za kiserikali zinazo toa mchango mkubwa katika suala zima la kuendeleza na kukuza
ujasiriamali kama vile SIDO, TEMDO, TCCIA na nyinginezo.
Nijukumu la kila
mwanajamii kuutambua mchango wa shughuli za ujasiriamali katika kuinua hali ya
uchumi wa nchi yetu Tanzania kwani hii ndo secta pekee inayotoa ajira kwa wananchi
katika kiwango kikubwa ukilinganisha na nyingine.
Sisi kama wasomi wa
elimu ya juu tukichukua shahada ya masoko na ujasiriamali katika chuo kikuu cha
ushirika na biashara Moshi, tungependa kuutambua mchango mkubwa inaoutoa serikali yetu katika kuukuza
ujasiriamali wa ndani,hii ni kwakuwa tumekuwa tikiona vyuo vinavyotoa elimu ya
ujasiriamali katika ngazi mbalimbali za elimu na ndo maana mpaka sasa tuko
katika chuo cha ushirika na biashara tukichukua elimu ya biashara.
Hatutakuwa tumetenda haki endapo tutazisahau taasisi au makampuni binafsi yanayotoa elimu ya ujasiriamali na ushauri wa kibiashara kwa lugha ya kigeni tunaziita Management consultant firms mfano: East Africa Productive Trainers (EAPTRAINERS), Beatruth Ltd, Multlevel Business Solution (MBS) ,nanyinginezo,taasisi hizi huchangia katika kiwango kikubwa kukuza fikra za watu wengi katika maswala yote yahusuyo fedha na uchumi hii ni kwakuwa hata sisi huku chuoni tunazitegemea sana huduma zao kwasababu kupitia wao tunapata kujua nijinsi gani mtu anaweza kujiajiri mwenyewe bila kutegemea kuajiriwa kama sehemu pekee ya ajira yake, lakini pia tunapata fursa ya kuhamasishwa kujikita katika ujasiriamali pale tunapoonyeshwa mafanikio wanayopata wajasiriamali licha ya changamoto nyingi zinazowakumba.
Tunawasihi sana watanzania wenzetu tupende ujasiriamali kwa ajiri ya ukombozi wa hali ya kiuchumi ya nchi yetu na kwa maendeleo ya watanzania kwaujumla
.
Makala haya yameandaliwa
na wanachuo wa chuo kikuu cha ushirika na biashara Moshi (MUCCoBS) ambao ni:
Richard Fernandes, Cathiline Shoo, Tendo T. Waida, Daniel Ngowi, Ramadhan Ally,
Andrew Anga, Deus Mwampiki, Peter Mbilinyi, Godsave Massawe, Mrisho Juma
Migessi na Robert Mshome
wanaochukua shahada ya masoko na ujasiriamali mwaka wa pili..
No comments:
Post a Comment