Monday, 19 May 2014

WANACHUO WA CHUO CHA USHIRIKA NA BIASHARA MOSHI (MUCCoBS) WAPATA ELIMU YA SOKO LA HISA

Wanachuo wa chuo cha ushirika na biashara Moshi (MUCCoBS) wamepewa elimu ya masuala ya soko la hisa kwa majina ya kigeni tunaliita stock exchange iliyowezeshwa na mtaalam kutoka Dar es salaam Stock exchange(DSE) Bw. Magebe, tulioudhuria tumeyapata mengi mazuri ya kuwaeleza wengine yakiwa ni pamoja na system au fursa mpya iliyopo kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo inayoendeshwa na DSE kupitia mitandao ya simu kama Airtel na Tigo.

System hii inampa mwanafunzi nafasi ya kujifunza zaidi kuhusu soko la hisa na jinsi ya kufanya biashara ya hisa ambapo atatafutwa mshindi atakayezawadiwa kiasi cha Tsh 1000,000/= baada ya zoezi kuisha ambaye atapatikana kwa kuangalia ametengeneza kiasi gani cha pesa katika biashara ya kununua na kuuza hisa katika taratibu atakazokuwa amepewa

Unaweza sasa kujiunga kwa kupiga *150*36# kwa wateja wa Airtel na Tigo kupata maelezo zaidi au wasiliana na Bw. Magebe kupitia 0788633677.

No comments:

Post a Comment