Monday, 19 May 2014

WANACHUO WA CHUO CHA USHIRIKA NA BIASHARA MOSHI (MUCCoBS) WAPATA ELIMU YA SOKO LA HISA

Wanachuo wa chuo cha ushirika na biashara Moshi (MUCCoBS) wamepewa elimu ya masuala ya soko la hisa kwa majina ya kigeni tunaliita stock exchange iliyowezeshwa na mtaalam kutoka Dar es salaam Stock exchange(DSE) Bw. Magebe, tulioudhuria tumeyapata mengi mazuri ya kuwaeleza wengine yakiwa ni pamoja na system au fursa mpya iliyopo kwa ajili ya wanafunzi wa vyuo inayoendeshwa na DSE kupitia mitandao ya simu kama Airtel na Tigo.

System hii inampa mwanafunzi nafasi ya kujifunza zaidi kuhusu soko la hisa na jinsi ya kufanya biashara ya hisa ambapo atatafutwa mshindi atakayezawadiwa kiasi cha Tsh 1000,000/= baada ya zoezi kuisha ambaye atapatikana kwa kuangalia ametengeneza kiasi gani cha pesa katika biashara ya kununua na kuuza hisa katika taratibu atakazokuwa amepewa

Unaweza sasa kujiunga kwa kupiga *150*36# kwa wateja wa Airtel na Tigo kupata maelezo zaidi au wasiliana na Bw. Magebe kupitia 0788633677.

Saturday, 17 May 2014

WAKULIMA WAFANYABIASHARA WAKUTANISHWA NA HASASI ZA KIFEDHA- ARUSHA


HATIMAYE MAONYESHO YA WAKULIMA (AGRI FINANCE FAIR 2014)- AVRDC, ARUSHA CHINI YA AGRI HUB TANZANIA YAMEFIKA TAMATI.

UONGOZI WA BENACHIKO ENTREPRENEURSHIP CONNECTION (BEC) UMEHUDHURIA MAONYESHO YALIYOKUWA YA KIPEKEE SANA KWANI YALIKUWA YANASHIKA HASA KATIKA SUALA LINALO WASUMBUA MAJASIRIAMALI WENGI LA MTAJI WA KUFANYIA BIASHARA KWANI MAONYESHO HAYA YALILENGA SANA KUWAKUTANISHA WAFANYABIASHARA WAKULIMA NA HASASI ZA KIFEDHA ZA SERIKALI NA ZA BINAFISI,YALIKUWA YA SIKU MBILI YAANI TAREHE 25 NA 26 APRIL. TULIOHUDHURIA TUMEFAIDI SANA KWA KUPEWA USHAURI JUU YA NJIA NZURI ZA KUPATA MIKOPO YA KUENDESHEA BIASHARA ZETU NA UTARATIBU WA MASOKO YA MAZAO YA KILIMO KWA KUWAUNGANISHA WAKULIMA NA HASASI ZINAZO JISHUGHULISHA NA MASOKO YA KILIMO , LAKINI PIA TUMEPATA ANUANI MPYA KWA USHIRIKIANO ZAIDI WA KIBIASHARA.



Monday, 12 May 2014

BENACHIKO ENTREPRENEURSHIP CONNECTION (BEC) IKITOA ELIMU YA UJASIRIAMALI


Mtaaramu wa masuala ya ujasiriamali na masoko Bw. Benami Faustine wa Benachiko Entrepreneurship Connection (BEC) akitoa elimu ya ujasiriamali kwa wajasiriamali maeneo ya Sanya juu wilaya ya Siha chini ya program ya Sustainable Land Management (SLM) iliyodhaminiwa na United Nations Development Program (UNDP) na kuwezeshwa na shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO)- Kilimanjaro