Neno mjasiliamali ni neno lililo ibuka miaka
ya 1400 katika enzi za akina Marco polo, Vasco Da Gama na Bartholomew Diaz na kushika kasi katika miaka ya 1700 katika
bara la ulaya na baadae sehemu nyingine za dunia Afrca ni miongoni mwa sehemu
hizo,hivyo basi mjasiliamali ni mtu anayeanzisha, anayesimamia na kundesha biashara huku akiwa na utayari wa kukabiliana na changamoto katika biashara yake.Kulingana
na usemi wa Mfaransa Richard Cantillon anayesema kuwa mjasiliamali ni mtu
anayenunua kitu(vitu) kwa bei
inayojulikana na kutarajia kuuza kwa bei fulani ambayo hana uhakika nayo kwenye soko.Na hapa ndipo mjasiliamali anasemekana kuwa ni mtu anayeweza
kuvumilia hasara kwani kitu(vitu) anachokwenda kuuza hana uhakika wa soko lake
na hata hajui atamuuzia nani, kwa bei gani na katika mazingira gani.
Pia
katika hali nyingine mjasiliamali ni mtu yoyote ambaye ni mugunduzi na mbunifu
katika bidhaa,katika njia mpya za uzalishaji ,njia mpya ya vikundi na
ushilikishaji pia njia mpya za masoko.Hivyo mjasiliamali hujiajili, hukabliana na changamoto chungu
nzima za kibiashara .
Kwa
mfano vijana hawaa katika picha chini ni wajasiliamali wadogo ambao wananunua miwa kutoka kwa wakulima wa miwa kwa bei
inayojulikana huku wakitegemea kuuza miwa kwa bei ambayo hawana uhakika nayo.
No comments:
Post a Comment