Wednesday 15 May 2013

MJASILIAMALI NI NANI?


            Neno mjasiliamali ni neno lililo ibuka miaka ya 1400 katika enzi za akina Marco polo, Vasco Da Gama  na Bartholomew Diaz na kushika kasi katika miaka ya 1700 katika bara la ulaya na baadae sehemu nyingine za dunia Afrca ni miongoni mwa sehemu hizo,hivyo basi mjasiliamali ni mtu anayeanzisha, anayesimamia na kundesha  biashara huku akiwa na utayari wa kukabiliana  na changamoto katika biashara yake.Kulingana na usemi wa Mfaransa Richard Cantillon anayesema kuwa mjasiliamali ni mtu anayenunua kitu(vitu) kwa bei  inayojulikana na kutarajia kuuza kwa bei fulani ambayo hana uhakika nayo kwenye soko.Na hapa ndipo mjasiliamali anasemekana kuwa ni mtu anayeweza kuvumilia hasara kwani kitu(vitu) anachokwenda kuuza hana uhakika wa soko lake na hata hajui atamuuzia nani, kwa bei gani na katika mazingira gani.
             Pia katika hali nyingine mjasiliamali ni mtu yoyote ambaye ni mugunduzi na mbunifu katika bidhaa,katika njia mpya za uzalishaji ,njia mpya ya vikundi na ushilikishaji pia njia mpya za masoko.Hivyo mjasiliamali  hujiajili, hukabliana na changamoto chungu nzima za kibiashara .
                       Kwa mfano vijana hawaa katika picha chini ni wajasiliamali wadogo ambao  wananunua miwa kutoka kwa wakulima wa miwa kwa bei inayojulikana huku wakitegemea kuuza  miwa kwa bei ambayo hawana uhakika nayo.

No comments:

Post a Comment