Saturday 6 July 2013

MAKALA YA UJASIRIAMALI YALIYOANDIKWA NA WANAFUNZI WA MASOKO NA UJASIRIAMALI MUCCoBS

              Ni kitu cha kujivunia katika jamii yetu ya kitanzania kuwa na taasisi mbalimbali zinazotoa mchango mkubwa katika kukuza ujasiriamali wa ndani zikiwemo zile zinazotoa mikopo nafuu kwaajiri  ya wajasiriamali wadogo taasisi za aina hii ni pamoja na SACCoS, FINCA, Na nyinginezo , lakini pia zipo nyingine zinazotoa misaada katika kusaidia kuwezesha miradi mikubwa ya ujasiriamali katika nchi yetu ya Tanzania kama vile taasisi zisizo za kiserikali (NGO’s) mfano Trias, na BESTAC  lakini pia zipo taasisi za kiserikali zinazo toa mchango mkubwa  katika suala zima la kuendeleza na kukuza ujasiriamali kama vile SIDO, TEMDO, TCCIA na nyinginezo.
Nijukumu la kila mwanajamii kuutambua mchango wa shughuli za ujasiriamali katika kuinua hali ya uchumi wa nchi yetu Tanzania kwani hii ndo secta pekee inayotoa ajira kwa wananchi katika kiwango kikubwa ukilinganisha na nyingine.

Sisi kama wasomi wa elimu ya juu tukichukua shahada ya masoko na ujasiriamali katika chuo kikuu cha ushirika na biashara Moshi, tungependa kuutambua mchango mkubwa  inaoutoa serikali yetu katika kuukuza ujasiriamali wa ndani,hii ni kwakuwa tumekuwa tikiona vyuo vinavyotoa elimu ya ujasiriamali katika ngazi mbalimbali za elimu na ndo maana mpaka sasa tuko katika chuo cha ushirika na biashara tukichukua elimu ya biashara.

Hatutakuwa tumetenda haki endapo tutazisahau taasisi au makampuni binafsi yanayotoa elimu ya ujasiriamali na ushauri wa kibiashara kwa lugha ya kigeni tunaziita Management consultant firms mfano: East Africa Productive Trainers (EAPTRAINERS), Beatruth Ltd, Multlevel Business Solution (MBS) ,nanyinginezo,taasisi hizi huchangia katika kiwango kikubwa kukuza fikra za watu wengi katika maswala yote yahusuyo fedha na uchumi hii ni kwakuwa hata sisi huku chuoni tunazitegemea sana huduma zao kwasababu kupitia wao tunapata kujua nijinsi gani mtu anaweza kujiajiri mwenyewe bila kutegemea kuajiriwa kama sehemu pekee ya ajira yake, lakini pia tunapata fursa ya kuhamasishwa kujikita katika ujasiriamali pale tunapoonyeshwa mafanikio wanayopata wajasiriamali licha ya changamoto nyingi zinazowakumba.

Tunawasihi sana watanzania wenzetu tupende ujasiriamali kwa ajiri ya ukombozi wa hali ya kiuchumi ya nchi yetu na kwa maendeleo ya watanzania kwaujumla
.

Makala haya yameandaliwa na wanachuo wa chuo kikuu cha ushirika na biashara Moshi (MUCCoBS) ambao ni: Richard Fernandes, Cathiline Shoo, Tendo T. Waida, Daniel Ngowi, Ramadhan Ally, Andrew Anga, Deus Mwampiki, Peter Mbilinyi, Godsave Massawe, Mrisho Juma Migessi na Robert Mshome
wanaochukua shahada ya masoko na ujasiriamali mwaka wa pili..

No comments:

Post a Comment